RSS

2010-KCSE-TRIAL-KISWAHILI-P3-001

09 Sep

KIS-OP3-001

102/3

KISWAHILI

Karatasi ya 3

(Fasihi)

Julai/Agosti 2010

MUDA: Saa Mbili (2)

Hati Ya Kuhitimu Elimu ya Secondari Kenya

Kidato cha Tatu

Kiswahili

Julai/Agosti 2010

Karatasi 3

Saa: 2

MAAGIZO:

1. Jibu maswali matatu pekee

2. Swali la kwanza ni la lazima

3. Maswali hayo mengine yachaguliwe kutoka sehemu zilizobaki: Yaani Tamthilia, Riwaya, Hadithi fupi na Fasihi simulizi.

4. Ujibu maswali mawili kutoka sehemu moja.

USHAIRI

Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata:

SHAIRI A

1) Mashekhe na mapadiri, najashitakia kesi,

Ya kuvamiwa kisiri, kwa moto ndifu na nyasi,

Maonevu yamejiri, yamenifika utosi,

Nimetenda kosa gani, hata nichomwe kwa moto?

2) Kukicha huwa mbioni, kasikazi hadi Kusi,

Kuzuru mizaituini, michungwa na mifenesi,

Ninapouya jioni nangojwa na ibilisi,

Nimefanya baya lipi, hata nichomwe kwa moto?

3) Mja nimemkosani, asiyenipa nafasi?

Lichwapo jua jioni, avizia kunighasi,

Kwa moto awashe kuni, utamdhani majusi,

Kutaka yangu asali, hata nichomwe kwa moto?

4) Makumbi yalokauka, atayawasha upesi,

Kwa ghafula ‘kishituka, moto ushanikorosi,

Wanangu humautika, nyoyo zikawa nyeusi

Nimefanya ovu gani, hata nichomwe kwa moto?

5) Hamuwachomi mainzi, walosheheni virusi,

Mbona hamwendi panzi, wazushao wasiwasi,

Hata na kwenye minazi, kuna mavu na mijusi,

Kosa langu nambieni, hata nichomwe kwa moto?

6) Mbelewele kuichuma, ni sulubu si rahisi,

Huchuma mikiwa wima, hakuna pa kujilisi,

Nyingine umeiuma, na miguu sitikisi,

Kisha milima nivuke, hata nichomwe kwa moto!

7) Kama ni yangu asali, inayonipa mikosi,

Basi twaeni kalili, kwa upole bila fosi,

Isiwe kwa ukatili, ukali pia kisasi,

Nimetenda ovu gani, hata nichomwe kwa moto?

8) Hata haya hawaoni, waja wamekuwa fisi,

Au asali wadhani, hatuihitaji nasi?

Basi koma na komeni, koma achaneni nasi,

Nimetenda kosa gani, hata nichomwe kwa moto?

9) Sitaondoka kortini, hadi muamue kesi,

Munipe lilo yakini, unitoke wasiwasi,

Tena aje kizimbani, tujadiri hino kesi,

Kosa langu anambie, hata nichomwe kwa moto?

SHAIRI B

Haifai,

Kumshambulia mkeo,

Kwa sababu umekandamizwa,

Na mtu usiyemuweza.

Haifai,

Kutaka uheshimiwa,

Na huheshimu wenzako,

Haifai, haifai, haifai,

Tena haifai.

Haifai,

Kujidunisha mwenyewe,

Sababu umedunishwa,

Itetee haki yako,

Hilo ndilo lafaa.

Haifai,

Kupiga watoto wako,

Mkewe mkikosana,

Au memewe vilevile.

Haifai,

Kusema umetosheka,

Na kumbe wasononeka,

Waishi kama mnyama.

Haifai, kutaka unynyekevu,

Pasipo kunynyekea,

Haifai, haifai, haifai,

Tena haifai.

Haifai,

Kungoja usaidiwe,

Bila kufanya lolote,

Tafuna unachopewa,

Singoje utafuniwe.

1) USHAIRI

a) Onyesha tofauti zozote za kimuundo kati ya shairi A na B. (Alama 6)

b) Watunzi wana dhamira gani? (Alama 4)

c) Andika ubeti wa saba (7) shairi A katika lugha nathari. (Alama 4)

d) Taja na utoe mifano ya mbinu mbili zilizotumiwa na mtunzi wa shairi B. (Alama 4)

e) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika mashairi A na B (Alama 2)

i) Ushanikorosi

ii) Wasononeka

HADITHI FUPI

K.W WAMITILA: MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE

2) Maudhui katika ngome ya nafsi na utenzi wa moyoni ni kama shilingi kwa ya pili. Fafanua kwa kutoa mifano mwafaka. (Alama 20)

3) Kwa kurejea hadithi ya mkimbizi (John Habwe). Onyesha athari za vita na utoe mapendekezo ya jinsi tunavyoweza kuimarisha umoja wa jamii.

RIWAYA – UTENGANO

4) Riwaya ya Utengano ni ya kisasi. Thibitisha. (Alama 20)

TAMTHILIA – KIFO KISIMANI

“Unajua nini, pombe haipendi tumbo tupu. Hupenda tumbo ambalo limewekwa matandiko mazuri.”

a) Nani alitoa kauli hii? Kwa nini? (Alama 2)

b) Pombe ilizuziwa na mtu fulani, nani? Na kwa nini? (Alama 4)

c) Pombe ilikuja pamoja na vitu kadhaa. Vitaje na kueleza umuhimu wa kila kimoja. (Alama 6)

d) Onyesha sadfa zinazojitokeza katika matukio ya muktadha huu. (Alama 6)

e) Kutokana na dondoo hili, onyesha udhaifu wa walinzi hawa. (Alama 2)

5) FASIHI SIMULIZI

a) Fafanua vipera hivi vya fasihi simulizi. (Alama 8)

i) Misimu

ii) Mighani

iii) Wawe/Vave

iv) Nyiso

b) Taja sifa za nyiso (Alama 4)

c) Eleza mbinu ambazo mtambaji wa hadithi atazitumia ili kuteka hisia za hadhira yake.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on September 9, 2010 in Kiswahili, Paper 3

 

Tags:

Comments are closed.

 
%d bloggers like this: