KIS-OP1-001
102/1
KISWAHILI
Karatasi ya 1
(Insha)
Julai/Agosti 2010
MUDA: 1 ¾
Hati Ya Kuhitimu Elimu ya Secondari Kenya
Kidato cha Tatu
Kiswahili
Karatasi 1
Muda: 1 ¾
MAAGIZO
1. Andika insha mbili
2. Insha ya kwanza ni ya lazima
3. Kisha chagua insha moja nyingine kutoka hizo NNE zilizobakia.
4. Kila insha isipungue maneno mia nne (400)
5. Kila insha ina alama 20.
1.
Wewe ni afisa wa kilimo wilayani. Andika shajara ya wiki moja.
2. Eleza jinsi serikali inavyoweza kutumia misaada ya kifedha kutoka nchi za ng’ambo.
3. Fimbo ya mbali haiui nyoka. Thibitisha ukweli wa methali hii.
4. Usawa wa kijinsia ni jambo lisilowezekana. Jadiri
5. Walipokaribia nyumbani, kwa ghafla alipigwa pigo kubwa kwenye kisogo. Alipogeuka alimwona yule mtu aliyejitolea kumpeleka nyumbani akijificha kitu kama rungu————-. Endeleza kisa hiki.